NA MWANDISHI WETU, LONGIDO
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Salum Kalli, amekabidhiwa hati ya heshima na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya kwa mafanikio ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2025.
Hati hiyo ilikabidhiwa Januari 30, 2026 na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Mhe. Papaa Nakuta Mollel, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido (JK Nyerere).
Katika hafla hiyo, Mhe. Kalli aliambatana na Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, waliokuwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya maendeleo kwa mujibu wa Ilani ya Chama
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: +255 272 970 793/ 94
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.