NA ABRAHAM NTAMBARA, LONGIDO
Mkuu wa Wilaya yaLongido, Mhe. Salum Kalli, ametoa siku 12 kwa vikundi vinavyodaiwa mikopo yaasilimia 10 ya Halmashauri vilivyokopa kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 kuhakikishavinarejesha mikopo hiyo.
Kauli hiyo ameitoaleo Januari 19, 2026, wakati akizungumza na vikundi hivyo katika ukumbi waHalmashauri wa JK Nyerere, ambapo amesema muda huo utaisha Januari 31, 2026.
Mhe. Kalli amesemakuanzia Februari 1, 2026, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwakushirikiana na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii watapita kikundi kwakikundi kuhakiki kiasi kilichokopwa na kilichorejeshwa.
Amesisitiza kuwa vikundi ambavyo havitakuwa vimerejesha mikopo hiyo vitachukuliwa hatua kali zakisheria.
“Lengo lakuwakopesha ni kuwasaidia mfanye maendeleo yenu, lakini ni lazima mrejeshe ilina wengine wapate. Mikopo hii inasaidia wananchi kuepuka mikopo ya kausha damu.Sasa kama mnakopeshwa na hamrejeshi, wengine watakopeshwa nini?” amesema Mhe.Kalli.
Hata hivyo, Mhe.Kalli amevitaka vikundi hivyo kutumia mikopo waliyopewa kwa malengoyaliyokusudiwa badala ya kugawana fedha hizo kwa matumizi binafsi yasiyohusianana shughuli za kikundi, jambo ambalo limekuwa chanzo cha kushindwa kurejeshamikopo kwa wakati.
Katika hatuanyingine, Mhe. Kalli amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaWilaya ya Longido kuwaandikia barua Watendaji wa Kata ili kuwapa maelekezo yakuwafahamisha Watendsji wote kufuatilia marejesho kwa vikundi vote vinavyodaiwa kwa ukaribu na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati
Kwa upande wake,Katibu Tawala wa Halmashauri hiyo, Bi. Rahma Kondo, amesema hakuna kikundikitakachosamehewa kurejesha mikopo hiyo, na kuvitaka vikundi kuacha kutoavisingizio vya kushindwa kurejesha mikopo kwa madai ya ukame, akieleza kuwabaadhi ya vikundi vilikopa wakati hakukuwa na ukame.
Amebainisha kuwakuna vikundi vinavyoendesha biashara kubwa na zinazoonekana wazi, lakini kwamakusudi vinashindwa kurejesha mikopo hiyo.
Mikopo ya asilimia10 ya Halmashauri haina riba na hutolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana nawatu wenye ulemavu kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: +255 272 970 793/ 94
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.