Kamati ya Fedha na Mipango Halmashauri ya Longido leo tarehe 27/02/2019 imehitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kumi na tano (15) kwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa ni utaratibu wa kisheria kwa kamati hii kutembelea miradi kwa kila robo.
Kamati imetembelea ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Tinga Tinga ,Ujenzi wa madarasa shule ya msingi Tinga Tinga,Ujenzi wa mabweni na madarasa shule ya sekondari Enduimet,Ujenzi wa kituo cha afya Ketumbeine,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Ketumbeine,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Flamingo,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Lekule sekondari,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Namanga,Ujenzi wa hospitali ya Wilaya.Ujenzi,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Namanga,Ujenzi wa madarasa shule ya msingi Orbomba,Mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Oltepes,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Engarenaibor,Ukamilishaji wa Ujenzi sekondari ya Matale, na ujenzi wa kituo cha Afya Engarenaibor.
Wajumbe wa kamati hiyo wametoa maagizo mbalimbali kwa miradi waliyokagua lakini wameridhishwa zaidi na ujenzi wa madarasa manne ya shule ya sekondari Tinga Tinga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi kuanzia msingi mpaka kufikia hatua ya umaliziaji yakiwa na kiwango cha juu na gharama ndogo.
Nao wananchi wa Tinga Tinga wameiomba serikali iwaangalie kwa jicho la pekee kwani hatua waliyofikia wanaomba washikwe mkono ukizingatia kwa sasa wana miradi mingine wanayotekeleza kwa nguvu za wananchi ikiwa ni mradi wa Zahanati na madarasa ya shule ya msingi yote yanajengwa kwa nguvu za wananchi.
Mh Diwani Naomi Mollel amewapongeza sana wananchi wa Tinga Tinga kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuwataka waendelee na moyo huo wa kuchagia miradi ya maendeleo, "Hakika juhudi yenu wanachi wa kata ya Tinga Tinga ya kuchangia miradi ya maendeleo ni kubwa sana kuliko kata yoyote katika halmashauri yetu,niwapongeze kwa hilo na sisi kama wajumbe wa kamati ya Fedha tunalibeba hili na kuliwasilisha katika kikao cha kamati ya Fedha kitakochokaa keshokutwa ili tuone namna gani tutawashika mkono ingawa kama Halmashauri tuna miradi mingi kila mahali lakini haiwezekani kwa juhudi zenu hizi tuwaache hivi hivi" alisema Mh.Naomi Mollel.
Nae Mh. Kenedy Sabore ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido akizugumza na baadhi ya wanakamati katika shule sekondari Engarenaibor amefurahishwa na mwamko wa wananchi kuchangia maendeleo ya kata zao ambapo kata ya Engarenaibor wamechangia madarasa mawili na ofisi moja na kata ya Mundarara wamechangia madarasa mawili na ofisi moja jumla madarasa manne na ofisi moja ambazo zote zipo hatua ya lenta."Ndugu wanakamati hongereni sana kwa kazi nzuri ya ujenzi wa madarasa katika kata zenu tunatambua umuhimu wa michango yenu katika uharakishwaji wa maendeleo ya kata zenu na wilaya kwa ujumla,ombi langu endeleeni na moyo huo huo wa kujitolea kwa ajili maendeleo ya wilaya yetu,pili kamati ya ujenzi mjitahidi kuwalinganisha mafundi wazoefu na wa bei nafuu ili kuweza kufikia malengo ya gharama iliyopo kwenye makisio ya mhandisi (BOQ) "alisema Sabore".
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM