Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Longido, wameidhinisha mpango wa bajeti ya mapato na matumzi kwa mwaka ujao wa fedha wa 2021/2022, wakati wa mkutano maalum wa Baraza la madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Longido.
.Wakizungumza wa wakati wa mkutano huo maalumu wa Baraza la Madiwani, wajumbe hao wameidhinisha mpango huo wa bajeti ambao, kimsingi umezingatia vigezo vya uandaaji wa bajeti pamoja na kugusa maeneo yote kisekta, huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni uboreshaji sekta ya elimu na Afya na Ardhi kwa ajili ya upimaji na kukusanya mapato ya ndani.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Longido, Mheshimiwa Saimon Oitesoi, amesema kuwa fedha hizo kiasi cha bilion 25.9 zimelenga zaidi katika kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa halmashauri ya Longido, licha ya kwamba bado halmashauri inakabiliwa na tatizo la kuwa na mapato kidogo lakini tumejipanga kusimamia na kukusanya mapato na kubuni vyanzo vipya vya Mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri akichangia rasimu ya Bajeti
Akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Afisa Mipango halmashauri ya Longido Peter Ngusa, ameweka wazi kuwa, halmashauri imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 25.9.
Afisa Mipango huyo amefafanua kuwa, utekelezaji wa bajeti hiyo ya shilingi bilioni 25.9, unategemea mapato ya ndani kwa shilingi bilioni 2,238 ,600,000.00, TZS761,086,000.00 fedha kwa ajili ya matumizi mengineyo, bilioni 10.2 ikiwa ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo huku ruzuku ya mishahara ya watumishi ikikadiriwa kutumia kiasi cha shilingi bilooni 12,695.487,600.00. Asilimia 90 ya bajeti inategemea serikali kuu.
Afisa Mipango wa Halmashauri Peter Ngusa akiwasilisha Rasimu ya bajeti mwaka wa Fedha 2021/2022.
Nae Mheshimiwa diwani wa kata Mundarara Alais Mushao akichangia rasimu hiyo amesema bajeti imegusa sekta zote muhimu changamoto ni ufinyu wa bajeti kutokana na kuwa na vyanzo vichache vya mapato lakini tumejipanga kuanzisha miradi mbalimbali itakayoongeza mapato ya Halmashauri yetu.
Mhe Alais Mushao diwani kata ya mundarara akichangi rasimu ya bajeti mwaka wa fedha 2021/2022
Rasimu hiyo ya mpango wa bajeti ya halmashauri ya Longido, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 licha ya kuidhinishwa na mkutano maalum wa Baraza hilo la Madiwani, bado inaendelea kuwa rasimu mpaka kukamiliaka kwa michakato yote ya kisheria na hatimaye kufikia kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuanza utekelezaji wake ifikap Julai 1, 2021.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM