Halmashauri ya Wilaya ya Longido imewasihi wahitimu wa kidato cha Sita kujiendeleza kimasomo wakati wanasubili matokea (post) za kuendelea na Elimu ya juu (vyuo vikuu) baada ya kumaliza mitihani kwa salama leo Mei 20, 2019.
Akitoa ufafanuzi huo ofisini kwake Afisa Elimu Idara ya Sekondari wa Wilaya hiyo Gerson Mtera amesema kuwa wanafunzi wote wa shule zote mbili yaani Longido Sekondari na Suma Engikareti wamemaliza mitihani salama na tumewasihi wasiende kukaa nyumbani badala yake waendelee kujisomea masomo mbalimbali ili kujiweka katika mazingira yaliyobora.
Aidha Mtera ametaja Somba ambalo wametilia mkazo kuwa ni somo la Kompyuta ambalo kila mmoja anapaswa kulifahamu kwa nyakati hizi amabzo nchi inapiga hatua “Tumewambia waende kusomo somo la Kompyuta maana ni la msingi na la kuleta ufanisi katika kazi zao watakazokuwa wanaendelea nazo hapo baadae na litawasaidia” amesema Mtera.
Hata hivyo swala la usimamizi wa mtihani hiyo Mtera amsema limefanyika vyema na Ofisi imejihakikishia kuwa amna udanganyifua wowote. Vilevile wasimamizi wa vituo vyote wameleta ripoti kamili ya kumalizika kwa mitihani na hapakuwepo na dosali zozote toka wanafunzi wameanza mitihani tarehe 6 mpaka wanamaliza Mei 20, 2019.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM