Mheshimiwa Esupati Ngulupa wa chama cha MAPINDUZI amechaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido baada ya kushika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja
Mh. Esupati Ngulupa ametetea kiti chake baada ya kupata kura 14 kati ya kura 23 zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Mhe. Naomi Mollel diwani viti maalum wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo( CHADEMA ) aliyepata kura 9
Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani na kufanya uchaguzi wa Makamu mwenyekiti wa baraza hilo ambapo kisheria huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido ndugu Jumaa Mhina amemtangaza Mh. Esupati Ngulupa ambaye ni Diwani viti maalum kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kupata kura 14 na kumshinda Mhe. Naomi Mollel aliyepata kura 9 kati ya kura 23 zilizopigwa.
"Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza mheshimiwa Esupati Ngulupa kuwa Makamu Mwenyekiti aliyepata kura 14 na kumshinda mheshimiwa Naomi Mollel aliyepata kura 9 kati ya kura 23 zilizopigwa na wajumbe wa baraza la Madiwani". Amesema Mhina.
Aidha Mh.Esupati Ngulupa amewashukuru wajumbe kwa kumpa kura zilizotosha kumpa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa baraza na kuahidi kufanya kazi na kila mmoja.
Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za serikali za mitaa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa baraza la Madiwani hufanyika kila baada ya mwaka mmoja na kufanya nafasi hiyo kugombewa kila baada ya muda huo kumalizika.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM