Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh Nurdin Babu leo tarehe 16./08/2021 ameongea na viongozi wa dini, Wenyeviti wa Vijiji, Mallaigwanani Watendaji wa vijiji na kata kuhusu mambo mbalimbali ya Maendeleo ya Wilaya yetu, Mh. Babu amewataka viongozi hao kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwani mitadi Mingi inatekelezwa kule na pesa nyingi serikali Inapeleka ngazi ya vijiji na kata, Lakini pia Mh Nurdin Babu amewataka viongozi hao kuimarisha ujiirani mwema na Nchi jirani na kuhamasisha kulipia ushuru wa Mifugo pindi wananchi wetu wanapopeleka mifugo yao nchi jirani kuuza
Vile vile Mh. Babu amewataka viongozi hao kuhamasisha na ukataji wa Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa inayogharimu elfu 30 kwa kaya moja ya watu 6 ambayo itakuwezesha kupata matibabu kuanzia Zahaniti Mpaka Hospitali ya Mkoa.
Afya ni Muhimu sana kwa maendeleo ya Nchi yetu hivyo mkate Bima ya Afya ya CHF ili muwe na uhakika wa' Matibabu pindi mnapoumwa, amesema Mh. Babu..
Mh.Babu Pia amewaambia viongozi hao wapate chanjo ya uviko 19 na kuhamasisha wananchi wore waliofikisha umri wa miaka 18 kupata chanjo ya uviko 19 kwani ugonjwa huu upo na unaua sana na amewahakikishi viongozi hao kuwa chanjo hii haina madhara yoyote ni chanjo kama chanjo nyingine tulizowahi kuchoma huko nyuma kama za surua, pepopunda, ndui na nyingine nyingi.Pia chanjo hiii ya uviko 19 itawasaidia pindi wanaposafiri nje ya Nchi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM