Shirika la kikistro lisilo la kiserikali la CONVOY OF HOPE(COH) limetoa msaada wa chakula kiasi Cha Tani 50 na Maharage Tani 18 Kwa ajili ya kaya zilizo athirika na ukame katika vijiji vya Emurtoto, Lesing'ita,na Mundara.
Mkurugenzi wa shirika la CONVOY OF HOPE ndugu Geofrey Mjema akikabidhi Chakula hicho Kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido amesema baada ya shirika kusikia taarifa ya tathimini iliyofanyika na kuonyesha Longido Kuna waathirika wa Janga la njaa shirika la CONVOY liliomba msaada kutoka makao makuu yaliyopo Marekani na msaada huo umepatika hivyo pokea Kwa ajili ya wananchi Hawa wa Longido,alisema Mkurugenzi Mjema.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Ng'umbi amelishukuru shirika la CONVOY Kwa msaada huo.
'Ninawashukuru sana shirika la CONVOY OF HOPE Kwa misaada yote mnayotoa Kwa jamii yetu, msaada wa Chakula,mifugo,mbegu na Kisima Cha maji ambacho Kijiji chote wanakunywa na wanafunzi wetu wanapata lishe bora Kwa kuwa na mboga za majani muda wote lakini pia Kwa kuwapatia taulo za kike ambazo zinawafanya watoto wa kike wahudhurie masomo yao bila shida,Sasa basi niwaombe wananchi muendelee na utaratibu wa kuwapatia watoto hawa chakula,taulo za kike hata baada ya shirika la CONVOY OF HOPE kumaliza mkataba wao, alisema Mh.Ng'umbi'
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM