Timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe leo tarehe 13/07/2020 wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Longido kujifunza jinsi Halmashauri ilivyoweza kupandisha Mapato ya Halmashauri kupitia mnada wa Mifugo na vyanzo vingine.
Timu hiyo imeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Adrian J.Jungu aliyeambatana na Afisa Biashara ,Afisa Mipango na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Momba.
Akiongea na ugeni huo Dkt Jumaa Mhina Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido amesema miaka minne nyuma Halmashauri ilikuwa inakusanya takribani milioni 540 kwa mwaka kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali lakini sasa tunakusanya wastani wa bilioni 2 kwa mwaka ambapo tunaweza kutoa asilimia kumi(10%) ya wanawake ,vijana na walemavu bila shida yoyote pia vikao vya waheshimiwa madiwani vinakaa kama ratiba inavyosema na tumeweza kuchangia fedha kwenye miradi ya Maendeleo,Pia tumeweza kupandisha mapato ya serikali kuu kupitia mnada huu wa mifugo wa eworendeke uliojengwa kwa ufadhili wa Programu ya MIVARF ambapo wizara ya Mifugo wamekusanya wastani wa bilioni 300 na Halmashauri tumekusanya takribani bilioni 1.2 kupitia mnada huu toka umeazishwa.
Mkurugenzi Mtendaji Dkt Mhina na wataalamu wa Halmashauri ya Longido akiongea na wataalamu kutoka Halmashauri ya Momba eneo la mnada Eworendeke.
Afisa Mifugo wa Halmashauri Ndugu Nestory Dagharo akiwaonyesha wageni hao jinsi mifugo inavyoingia na kutoka kwenye mnada huo
Pia timu hiyo imeweza kutembelea kiwanda cha kuchakata nyama kinachojengwa na mwekezaji Elia food overseas,wakiwa kiwandani hapo Dkt Mhina alisema kiwanda hiki kikikamilika Halmashauri inategemea kupata mapato kutokana na kodi ya huduma na tutaweza kutekeleza Miradi yetu ya Maendeleo lakini pia serikali kuu itapata mapato alisema Dkt Mhina.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Momba Ndg Adrian Jungu amemshukuru Dkt Mhina kwa ziara yao yenye mafanikio makubwa na kusema hakika ni Wilaya ya Mpakani inayofaa kuigwa na Halmashauri za mpakani.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM